Na Mwandishi wetu,Ruvuma.📍
KAYA zaidi ya sita katika kata ya Mtyangimbole wilaya ya Madiba Mkoa wa Ruvuma wamelalamikia uongozi wa kijiji cha Gumbilo kwa kuwapora maeneo yao kwa madai kuwa wanampatia mwekezeji.
Wana kaya hao wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema kuwa wameshangazwa na kitendo cha watu kuvamia maeneo yao na kuanza kufyeka miti huku wakidai eneo hilo lente ukubwa wa zaidi ya hekari 2000 ni mali ya mwekezaji na amepewa na uongozi wa kijiji cha Gumbilo.
Mmoja wa walalamikaji aliyejitambulisha kwa jina la Madigija Moku amesema kuwa ameshangazwa na kitendo cha kuona wanafamiwa na watu ambao siyo wenyeji wa kata ya Mtyangimbole na wala hawajulikani.
Moku anasema kuwa baada ya watu ambao hawafaamiki maeneo hayo na kuvamia na kuanza kufyeka miti ambayo wananchi hao waliitunza ikiwa ni sehemu ya kutekeleza matakwa ya serikali ya kutunza mazingira walijaribu kuwauliza kuwa ni kwanini wanafanya hivyo lakini wavamiaji walisema kuwa wanakofyeka ni mali ya mwekezeji ambaye ameuziwa na uongozi mtaa wa Gumbilo.
Kwa upande wake Mikembo Mwita amesema kuwa yeye ni mmiliki wa maeneo hayo zaidi ya miaka 10 kwa vibari maalumu kutoka katika kata ya Mtyangimbole na tumekuwa tukishiriki katika masuala yote ya kimaendeleo lakini cha kushangaza leo hii tunavamiwa kwa madai kuwa maeneo yao yamechukuliwa na mwekezaji.
"Mimi nipo hapa Mtyangimbole zaidi ya miaka 10 sasa na tunashiriki katika masuala yote ya kimaendeleo,na hatujawahi kuitishwa mkutano kwa ajili ya kututaka tutoe maeneo yetu kwa mwekezaji na wala hatujawahi kulipwa fidia.
"Sasa leo hii kijiji cha Gumbilo kinakuja katika kata ya Mtyangimbole kuuza maeneo yetu kwa madai kuwa ni mwekezaji sisi mwekezaji hatumjui na kibaya zaidi wamekuja vijana na misumeno ya umeme wamefyeka miti ambayo tumeitunza kwa muda mrefu sana.
"Kutokana na hali hiyo tunaiomba serikali kupitia kwa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuingilia kati mgogoro huu kwani kunaweza kusababisha machafuko"Mwita.
Wanaodai kuvamiwa katika maeneo hayo kwa madai kuwa ni sehemu ya Mwekezaji ni Madigija Moku,Mikembo Mwita,Tale lutala.
Wengine ni pamoja na Nkingwa pawa,Shija malulu,Tale lutala,Nkingwa pawa,Shija malulu na Ngasa Bangili.
Alipotafutwa mwenyekiti wa kijiji cha Mtyangimbole Henrick Lwambano ili aweze kutolea ufafanuzi malalamiko ya wananchi wake kuporwa maeneo ya na kupewa mwekezaji mwenyekiti huyo alisema hata anasikia kuwepo kwa mambo hayo lakini yeye kama kiongozi wa kijiji hajatoa hidhini ya kuuza maeneo.
"Utaratibu wa kutoa maeneo kwa mwekezaji ni lazima kuitisha mkutano wa kijiji na nilazima kuwepo na makubaliano ya kimaandishi kwa maana ya mktasari lakini hilo halijafanyika.
"Cha kushangaza hilo eneo wanalosema amepewa mwekezaji lipo Mtyangimbole na wala siyo gumbilo na wanaodaiwa kumpatia mwekezaji ni viongozi wa Gumbilo na niliposikia hayo niliagiza zoezi la kufyeka msitu lisitishwe mara majoa"ameeleza Mwenyekiti wa Mtyangimbole.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Gumbilo ambao ndo walalamikiwa kwa kuuza maeneo ya wananchi,aliyefahamika kwa jina moja la Vicent alipotafutwa ili atoe ufafanuzi juu ya tuhuma hizo alisema kuwa suala hilo analijua lakini kwa muda huo yupo katika kikao.
Juhudi za kuendelea kupata ukweli juu ya jambo hilo alitafutwa Afisa Mtendaji wa Gumbilo,Mwanaisha Omary, ili kutoa ufafanuzi amesema kuwa siyo kweli kuwa kijiji kimeuza maeneo hayo kwa mwekezaji.
Mwanaisha anaeleza kuwa waliomuuzia mwekezaji ni wananchi wnyewe waliokuwa na maeneo yao kwa muda mrefu na walikuwa hawajayaendeleza.
"Wananchi wenyewe ndio waliouza maeneo yao sisi kama Serikali tulikuwa tunasaidia wananchi kufuata taratibu na serikali ya kijiji kama kawaida ilikuwa inasimamia asilimia 10 ya mauziano kati ya muuzaji na mwekezaji.
"Pia wapo baadhi ya wananchi ambao wana maeneo katika maeneo hayo lakini bahati mbaya hawajafuata taratibu za kupata maeneo na nimekuwa nikiwahita ili wafike ofisini kwa lengo la kutimiza taratibu lakini hawafiki ofisini kwangu"ameeleza mwanaisha.
Alipotafutwa msimamizi wa anayetajwa kuwa mwekezaji aliyefahamika kwa jina la Ally hakuweza kupatikana wala kupokea simu yake ya kiganjani.



