Leo Jumatatu ya tarehe 13.04.2026 Mkuu wa Zimamoto wilaya ya Bahi A/Insp Mussa Msengi amemkabidhi Mkuu wa wilaya ya Bahi *Mhe; Joacim Thobias Nyingo* Mtambo wa Maokozi ikiwa ni ishara ya kupokelewa kwake na kuanza rasmi shughuli za uokoaji ndani ya wilaya ya Bahi
Makabidhiano hayo yamefanyika mbele ya wajumbe wa Kamati ya Usalama, Mkurugenzi pamoja na CMT, wakuu wa taasisi za Umma (Ruwasa, Duwasa, Tarura, Tanesco, watendaji Kata, viongozi wa dini pamoja na baadhi ya wananchi
Baada ya makabidhiano hayo, Mhe; Mkuu wa wilaya ameongea na hadhira iliyokusanyika katika viwanja vya Halmashauri ya wilaya ya Bahi ambapo ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi mahiri wa *Dkt. Samia Suluhu Hassan* kwa kuliwezesha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuwa na vitendea kazi vya kutosha na vya kisasa. Aidha amemshukuru Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa uongozi wake mahiri ambao umewezesha kuishawishi serikali ya awamu ya sita kuweza kufanikisha upatikanaji wa vifaa mbali mbali vya kizimamoto
Mhe; Joacim Thobias Nyingo hakusita pia kumshukuru Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma *SSF Rehema J Menda* kwa kuiteua wilaya ya Bahi kuwa miongoni mwa wilaya za mwanzo kupata mgao wa mitambo ya kizimamoto, " _Natambua kuwa mitambo hii haijafika ya kutosha wilaya zote lakini Bahi imeonekana inafaa kuwa ya mwanzo katika mgao wa vifaa hivi vya kisasa"_ wito wangu tuutunze mtambo huu ili kuweza kuhudumu kwa muda mrefu katika wilaya yetu.
Aidha amemwomba *Mkuu wa Zimamoto wilaya ya Bahi A/Insp Mussa Msengi* kushirikiana kwa karibu zaidi ina idara zote ndani ya wilaya ili iwe rahisi kutoa huduma zenye weledi wakati wote
Mhe; Mkuu wa wilaya ameupokea mtambo huo na kuujaribu kama ishara ya kuuzindua rasmi kwaajili ya kuanza kufanya kazi wilayani
Katika makabidhiano hayo Baba Mchungaji, *Rev. Can Nasson Mjimbu* kutoka kanisa la Anglican alipata fursa ya kufanya maombi kwaajili ya kupata baraka na ulinzi wake Mwenyezi Mungu ili kukidumisha chombo hiki kiweze kuwahudumia wananchi vyema lakini pia kuwalinda na kuwabariki wapiganaji watakao kuwa wanautumia mtambo huu kwa kuwahudumia wana Bahi na watanzania kwa ujumla
ZMM 0468 FC AHMED OMARY
*CPR III DODOMA*
🚨Subscribe YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA.






