Na Mwandishi wetu Dodoma 📍
April 15 2026.
Wananchi wa Mtaa wa Chinyoyo kata ya kilimani Jijini Dodoma wako hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu kutokana na kampuni inayokusanya taka katika Mtaa huo kuziacha takataka kwa muda mrefu bila kuziondoa jambo linalooelekea taka kuzagaa katika maeneo mbalimbali mtaani hapo.
Camera ya kituo hichi imefanikiwa kunasa picha mbalimbali za taka hizo kwenye baadhi ya maeneo ya Mtaa huu taka zikiwa zimezagaa zaidi ya miezi miwili na nusu katika Mtaa huo wa chinyoyo kata ya kilimani Jijini Dodoma.
Wakizingumza na kituo hichi wamesema kuwa kampuni yenye dhamana ya kuchukuwa taka hizo imeacha kwa muda mrefu Sasa jambo ambalo ni hatari kwa watoto wanaocheza kuweze kupata magonjwa ya mlipuko
"Tunajiuliza kwanini kampuni hiyo imeziacha taka hizi kwa muda mrefu Sasa huku tukiwa tunawalipa fedha ya kubeba taka hizo"alihoji mwananchi moja ambaye hakutaka kujulikana kwa jina lake.
Kituo hichi kilimtafuta Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Chinyoyo Mhe Faustina Bendera kutaka kujua undani wa jambo hili ambalo limekuwa kero kwa wananchi wa Mtaa huo.
Mwenyekiti Faustina amesema ni kweli kumekuwa na changamoto ya uchafu kuzagaa katika maeneo mbalimbali ya Mtaa wake ila tayari alishawasiliana na meneja wa kampuni hiyo ya usafi na Sasa wanalifanyia kazi japo shida kubwa ni miundombinu ya barabara za mtaa huo kuwa mbovu hasa katika kipindi cha masika hivyo magari yao kushindwa kuingia na kupita katika Mtaa huo kuchukuwa takataka hizo.
"Swala hili la kutokuwa na miundombinu mibovu ya barabara zangu za Mtaa limekuwa sugu tumezunguka sana katika kutoa taarifa ya ubovu wa miundombinu ya barabara za mtaa katika ofisi za wakala wa barabara za Mjini na vijijini Tarura lakini hakuna mafanikio pia meneja wa wakala wa barabara za Mjini na vijijini Tarura Mhandisi Emanuel Mfinanga alifika kujionea jinsi miundombinu hiyo ya barabara za mtaa wetu zilivyo haribika na kutuahidi kuangalia bajeti yake ili aje azifanyie marekebisho katika kipindi cha kiangazi kwakuwa wakati wa masika hawata weza"amesema Mhe Mwenyekiti Faustina
Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa huu amewataka Wananchi kuhakikisha kuwa Sasa taka zao zote wazitoe majumbani na kuhakikisha wanaziweka katika maeneo maalumu ambapo walau gari la taka linaweza kupita kiurahisi ili waweze kuzibeba taka hizo huku akiwaasa wazazi kuhakikisha watoto wao hawachezi katika maeneo ambayo wameweka taka hizo ili kuepuka kupata magonjwa.
Kwa upande wake Afisa mazingira wa halmashauri ya Jiji la Dodoma Dickson Kimaro amesema jambo la kusomba takataka hizo ni wajibu wa kampuni waliyoingianayo mkataba wa kisheria katika halmashauri ya Jiji la Dodoma ili kuhakikisha mji unakuwa safi.
"Kwa hili la Mtaa wa Chinyoyo kata ya kilimani Jijini Dodoma tayari Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa huu Mhe Faustina Bendera aliniambia juu ya changamoto hiyo na tayari nimeshawaelekeza viongozi wa kampuni hiyo kwenda kuzitoa takataka hizo haraka ili kuhakikisha mtaa huo unakuwa safi na salama katika kipindi hichi" amesema Afisa mazingira wa halmashauri ya Jiji la Dodoma Dickson Kimaro.
Afisa mazingira wa halmashauri ya Jiji la Dodoma Dickson Kimaro amesema Swala la usafi wa mazingira linaanzia nyumbani kwako kwa kuhakikisha utunzanji na usafi wa mazingira unaanzwa na mwenyewe kuhakikisha mazingira yanakuwa safi.


