Na Wellu Mtaki, Dodoma📍
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amewataka watumishi wa sekta ya ujenzi nchini kufanya kazi kwa bidii, weledi na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma kwa kuepuka vitendo vya rushwa pamoja na matumizi mabaya ya ofisi, ili kuongeza tija katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Akizungumza leo jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Ulega alizitaka taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kuongeza uwajibikaji, ufanisi na nidhamu ya kazi ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.
Aidha, alisisitiza umuhimu wa taasisi hizo kuwasilisha kwa wakati taarifa za utendaji wa bodi zao, akibainisha kuwa kwa mujibu wa sheria, taarifa hizo zinapaswa kuwasilishwa angalau miezi mitatu kabla ya kumalizika kwa mwaka wa fedha.
Sambamba na hayo, ameiagiza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kuongeza juhudi katika kusimamia miradi ya miundombinu ya barabara na viwanja vya ndege ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
🚨Subscribe YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA


