Na Jasmine Shamwepu Dodoma.📍
Waziri wa Afya Mohamed Mchengerwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mbio za Marathon Maalum zinazofanyika Jijini Dodoma ambapo Jumla ya Shilingi milioni 100 zinatarajiwa kukusanywa kwa ajili ya kuwasaidia wakunga na wauguzi wanaotoa huduma katika vyumba vya upasuaji.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Machi 22,2026 Jijini Dodoma,Msajili wa Baraza la Uuguzi na ukunga Tanzania(TNMC) Agnes Mtawa amesema lengo la mbio hizo ni kukusanya fedha kwa ajili ya kuwajengea uwezo wauguzi na wakunga pamoja na wataalam wengine wa Afya wanaotoa huduma vyumba vya upasuaji na katika halmashauri na vituo vya afya.
Mtawa amesema mbio hizo zitahamasisha utoaji huduma kwa kuzingatia maadili ya kitaaluma ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma yenye kuzingatia heshima na utu,pia ni sehemu ya mazoezi katika kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza.
"Marathon itahusisha wakimbiaji kwa KM 5,10,na 21 na inatarjiwa kuwa tukio kubwa la kimichezo likijumuisha takriban wakimbiaji 2000 ambao Kila mmoja atashiriki kwa mchango wa 30000 na tunatarajiwa kukusanya kiasi Cha Shilingi milioni 100"Amesema Agnes Mtawa
Hata hivyo amesema Malengo ya mbio hizo ni kuboresha utoaji huduma kwa wananchi,kujengea uwezo kwa wataalam wanaotoa huduma katika vyumba vya upasuaji ikiwemo kuwakutanisha na wadau mbalimbali wa sekta ya afya.
