UPENDO WA WANAWAKE WA DODOMA GLAMS GIRLS: MSAADA WAFIKA HADI HOSPITALI YA MIREMBE.


 Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
📍

Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, kikundi cha Dodoma Glams Girls kimetoa msaada kwa wanawake wenzao wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Mirembe, jijini Dodoma.


Akizungumza wakati wa tukio hilo, Mwenyekiti wa kikundi hicho, Happiness Njamasi, amesema lengo la msaada huo ni kuwafariji na kuwasaidia wanawake wenzao waliolazwa hospitalini hapo, ili kuwapa faraja na kuwafanya wajisikie kuthaminiwa katika kipindi hiki cha maadhimisho ya siku ya wanawake.


Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Dodoma Glams Girls, Juliana Kilua, amewaeleza waandishi wa habari kuwa misaada hiyo imepatikana kupitia michango iliyokusanywa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za kikundi hicho cha Dodoma Grand Girls.


Naye Mhasibu wa kikundi hicho, Harieth Ndugulu, ametoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kuchangia chochote walicho nacho pamoja na kujiunga na kikundi hicho ili kuendelea kusaidia jamii, hususan wanawake wenye uhitaji.


Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yamekuwa fursa kwa makundi mbalimbali kuonesha mshikamano na kusaidia jamii, hasa makundi yenye uhitaji maalum.



🚨 Full VIDEO Inapatikana Katika YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA.
Previous Post Next Post