Na Barnabas Kisengi, Dodoma.📍
Wafanya biashara za vyakula katika kata ya kilimani na mitaa yake minne wameaswa kuto kupandisha bei ya bidhaa katika kipindi hichi Cha mifungo ya mwezi mtukufu wa ramadhani na kwaresma.
Wito huo umetolewa na Diwani wa kata ya kilimani Mhe Mussa Mkunda alipokuwa akizungumza na kituo hichi katika mifungo ya mwezi mtukufu wa ramadhani na kwaresma inayoendelea hivi Sasa.
"Niwaombeni wafanya biashara wote wa maduka ya vyakula, hoteli na migahawa msiwapandishie wananchi bei ya bidhaa na vyakula katika kipindi hichi cha ambapo waumini wa dini zote wanatafutwa kupata thawabu na toba kwa mwenyezi Mungu"amesisitiza Mhe Mkunda
Aidha Diwani Mussa Mkunda amesema kuwa wafanya biashara wengi wamekuwa na Tabia ya kupandisha bidhaa za vyakula katika kipindi hichi jambo ambalo halileti tija kwa wananchi bali linakuwa linawaumiza wananchi wasio na uwezo wa kumudu kutafuta bidhaa za vyakula.
Mhe Mkunda pia ametumia nafasi hii kuwaasa wananchi katika kipindi hichi cha mvua zinazoendelea kunyesha kuhakikisha wanatunza mazingira kwa kufanya usafi wa mara kwa mara na kuhakikisha taka wanaziweka sehemu sahii ili kuweza kujiepusha na magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu.
Mhe Mkunda amewataka wakristu wote Mfungo mwema wa kwaresma na kwa waisilam wote Mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani huku akiwataka kuhakikisha wanajali ibada na kuwasaidie wasiojiweze,wazee na makundi maalumu ya watu wenye ulemavu ili waweze kupata thawabu za mwenyezi Mungu.
🚨Subscribe YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA.






