Na Barnabas Kisengi Dodoma. 📍
February 28 2026
Hatimaye ndoto ya wananchi wa mtaa wa chinyoyo kata ya kilimani Jijini Dodoma yakutokuwa na ofisi ya Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa kwa muda mrefu Sasa imeanza kuleta matumaini baada ya Wananchi wa mtaa huo kuanza kuchimba msingi wa ofisi hiyo na kuendelea kuhakikisha wanainua boma la ofisi hiyo kwa nguvu zao wenyewe ili kuweza kuhakikisha wanapata huduma za serikali wakiwa karibu kwenye mtaa wao.
Wakizungumza wakati wa zoezi la uchimbaji wa msingi wa ofisi hiyo baadhi ya wananchi wamesema kuwa wamekuwa wakipata shida mara nyingi kupatiwa kwa kukosa ofisi hivyo imekuwa ikiwalazimu mara kwa mara kumfuata Mwenyekiti nyumbani kwake au kwenda kwenye ofisi ya mtendaji wa kata ambayo iko katika mtaa mwingine hivyo huwagarimu kutumia usafiri wa Bodaboda au Bajaji jambo ambalo wanakuwa wakitumia Pesa nyingi ila Sasa kwa ujenzi wa ofisi hii utawarahisishia upatikanaji wa huduma wakiwa mtaani hapa.
Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Chinyoyo kata ya kilimani Mhe Faustina Bendera amesema katika jambo lililokuwa likimkera kwa muda mrefu Sasa limepata ufumbuzi wa ujenzi wa ofisi hiyo ambayo itasogeza huduma kwa ukaribu kwa Wananchi wa mtaa wake.
"Nikweli kama Mwenyekiti kukosa ofisi ya mtaa ilikuwa ni kero kubwa kwani wakati mwingine wananchi wanakuja nyumbani ili wapate huduma hata kama ulikuwa unapika au unafua inabidi uache kwanza umsikilize mwananchi na shida nyingine lazima uache kazi za nyumbani na utoke kwenda ukuwasaidia katika maeneo yao"amesema Faustina
"Nikiangalia tangu nakuwa hadi nimeingis madarakani tumekuwa tukifanya kazi za serikali ya Mtaa katika mazingira magumu maana hata watendaji wa mitaa tunao letewa wanashindwa kufanya kazi kwa utulivu kwa kukosa ofisi hivyo inawalazimu waende kukaa kwenye ofisi ya mtendaji wa kata hivyo Wananchi wakitoka kwangu inawalazimu kwenda kumfuata Mtendaji wa mtaa kwenye ofisi ya kata ila Sasa kwa ujenzi huu wa ofisi tunaamini huduma itakuwa karibu na wananchi wa mtaa wangu kwakuwa hapo ofisini nitakuwepo Mimi Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa na mtendaji wa Mtaa hivyo huduma zitapatikana kiurahisi sana hapo mtaani"alistukiza Faustina
Aidha Mwenyekiti Faustina amesema Jengo hilo linajengwa kwa kupitia nguvu za wananchi wenyewe pamoja na kusaidiwa na wadau mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo la Mtumba na waziri wa madini Mhe Anthony Mavunde yeye amewaza kuwashika mkono kwa kuwapatia matofali ya block elfu moja na mifuko ya saruji hamsini ambayo inaungana na nguvu za Wananchi waliyokubaliana kwenye vikao vya serikali ya Mtaa kila kaya itachangia Tsh elfu Tano ili kuhakikisha wamesimamisha ujenzi boma hilo kwa hatua za awali kwa kutumia nguvu za wananchi wa mtaa huo.
Awali akishiriki katka kuchimba msingi wa ofisi hiyo ya Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Chinyoyo kata ya kilimani Diwani wa kata ya kilimani Mhe Mussa Mkunda amewapingeza wanachi kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo na pia kwa kujitoa kwao kwa kuanzisha ujenzi wa ofisi hiyo kwakuwa wameonyesja jambo la kizalendo sana kwa kuanza kuchangia mchango wa Tsh elfu tano amesema hakika katika kaya elfu tatu za mtaa wa chinyoyo wakikamilisha kaya zote watakiwa wamekusanya kiasi cha Tsh milioni 15 ambayo watakiwa wamepiga hatua nzuri sana katika ushirikishwaji wa kusaidiana na serikali ya awamu ya sita katika kuleta marndeleo.
"Licha ya kuwapongeza niwaambie tu kama Diwani wa kata hii na mkazi wa Mtaa huu wa chinyoyo tutaku bega kwa bega hadi tukamilishe hapo tutakapo fikia na nikiwa kama mwakilishi wenu wa kata nitapambana hapo halmashauri ya Jiji kuhakikisha mtakapo fikia basi serikali itatusaidia kutakapo bakia kwakuwa mmeonyesha uwezo mkubwa wa kujitolea"amesisitiza Mhe Mkunda
Ujenzi huo wa ofisi ya Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Chinyoyo imeanza leo February 28 kwa kujitokeza wanchi wa Mtaa huo na kuanza kuchimba msingi kwa mamoja na kushirikiana na mafundi watakao jenga jengo hilo la ofisi ya Mtaa huu.







