Mtwara.📍
Wananchi walio na changamoto ya ugonjwa wa vikope(Trakoma) Wilayani Tandahimba Mkoani Mtwara wamenufaika na kambi ya Madaktari Bingwa wa Usawazishaji wa vikope .
Kambi hiyo imeanza leo tarehe 21,Januari,2026 katika Kituo cha Afya Mtakatifu Joseph Luagala Wilayani Tandahimba Mkoani Mtwara kwa uratibu wa Wizara ya Afya,Idara ya Kinga, Mpango wa Taifa wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele kwa kushirikiana na Kongwa Trachoma Project(KTP)
Wakizungumza mara baada ya kupata huduma hiyo, baadhi ya wananachi hao wameishukuru serikali kwa kutoa matibabu bila malipo kwenye jamii yao.
"Badala ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma lakini tumefuatwa kijijini kwetu tena bila malipo,tunashukuru sana"amesema Mwanahamis Juma.
Aidha, wameishukuru serikali kwa kuendelea kutoa elimu ya afya namna ya kujikinga na magonjwa mbalimbali ikiwemo vikope.
🚨Subscribe YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA.
