Na Jasmine Shamwepu Dodoma.📍
Upungufu wa walimu wa michezo, hususan walimu wa soka wa ngazi ya Diploma C, umeendelea kuwa changamoto kubwa nchini, hali inayochochewa na idadi kubwa ya watoto na ongezeko la vituo vya kukuza na kulea vipaji.
Akizungumza wakati wa mafunzo ya walimu wa soka yaliyoandaliwa na chama cha Makocha mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na chama cha soka mkoani humo Dorefa Luhaga Makunja amesema kuwa kwa sasa mkoa wa Dodoma una walimu wa Diploma C wasiopungua 100 huku akitaja idadi hiyo ni ndogo ukiringanisha na mahitaji.
Amesema kuwa makadirio ya kitaifa idadi ya walimu wa soka wa ngazi ya Diploma C nchini kote inaweza kuwa chini ya 2,000, hali inayoonyesha pengo kubwa la mahitaji ya walimu ukilinganisha na idadi ya vipaji vya watoto waliopo.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki katika kozi hiyo akiwemo Shabani Maganga na ignas Luhena ambao wanasomeshwa na Taasisi zao wameeleza ninkwa namna gani watatumia Taaluma waliyoipata kwenda kunyanyua vipaji.
🚨Full Video Inapatikana Kwenye YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA



