SERIKALI YA AWAMU YA SITA YAPITISHA SHERIA MPYA YA UNUNUZI WA UMMA, PPRA YATOA ELIMU KWA WANAHABARI

 


Na Carlos Claudio, Dodoma.📍


Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanikiwa kupitisha Sheria mpya ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2023 pamoja na Kanuni zake za mwaka 2024, hatua inayolenga kuongeza uwazi, uwajibikaji na matumizi sahihi ya fedha za umma.


Akizungumza leo Desemba 23, 2025 jijini Dodoma wakati wa semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa mkoa wa Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa PPRA, Bw. Dennis Simba, amesema ununuzi wa umma ni mchakato muhimu unaogusa kati ya asilimia 60 hadi 70 ya bajeti ya serikali, hivyo ni lazima uongozwe na sheria madhubuti.




Bw. Simba amesema semina hiyo imelenga kuwawezesha waandishi wa habari kuelewa kwa kina utekelezaji wa sheria ya ununuzi wa umma, kanuni zake ikiwemo GN namba 518 ya mwaka 2024 pamoja na matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa NeST katika ununuzi wa umma.


Amesisitiza kuwa PPRA imeona umuhimu wa kuwashirikisha waandishi wa habari ili waweze kuripoti kwa usahihi na weledi zaidi, kwani wao ni kiungo muhimu cha kuwafikishia Watanzania taarifa sahihi kuhusu jitihada na mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuharakisha maendeleo ya taifa.


Kwa mujibu wa PPRA, ushirikiano huo utaongeza uelewa wa umma na kuimarisha imani ya wananchi katika mifumo ya ununuzi wa umma nchini.






🚨Subscribe YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post