Na Mwandishi Wetu, WMTH, Mbeya.
Zoezi la uhakiki wa anwani za makazi linaendelea katika kata na mitaa ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma muhimu kwa wananchi kupitia utambuzi sahihi wa makazi.
Msimamizi wa zoezi hilo katika kata za Sisimba, Forest na Mabatini, Bi. Beatrice Makoko, amesema wananchi wanashirikishwa kwa karibu kupitia viongozi wa mitaa ili kurahisisha utekelezaji, na inapotokea mmiliki wa nyumba hayupo, taarifa zinaweza kutolewa na mtu wa karibu ili kuhakikisha kila nyumba inasajiliwa.
Mwakilishi wa afisa mtendaji wa kata ya Mbalizi Road, Bw. Raymond Gerald, amesema hadi leo Septemba 27, 2025 tayari nyumba zaidi ya 70 zimesajiliwa katika mitaa ya Kabisa, Kisoki, Mwasyoge na Sabasaba.
Zoezi linaendelea katika mitaa yote ya Jiji la Mbeya hadi kila kaya na taasisi zitakapohesabiwa na kusajiliwa rasmi.
🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.


