CHATANDA AMUHAKIKISHIA DKT. NCHIMBI KURA ZA KISHINDO KUTOKA KWA WANANCHI WA UBUNGO, WANASUBIRI KUTIKI OKTOBA 29.


Dar Es Salaam.📍

Mratibu wa Kampeni za CCM Jijini DSM ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) amemuhakikishia Mgombea Mwenza Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa Wananchi wa Jimbo la Ubungo wako tayari kumheshimisha Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Kumpigia kura za kishindo na kuibuka na ushindi Mkubwa kwenye Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025.


Akioongea kwenye Mkutano huo wa Kampeni Leo Tarehe 29 Septemba, 2025, kwenye Jimbo la Ubungo Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake wa chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) ndg. Mary Pius Chatanda amesema Wananchi wa Jimbo la Ubungo hususani Wanawake wako tayari kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la upigaji kura na kuhakikisha Dkt. Samia suluhu Hassan, pamoja na Mgombea ubunge wa jimbo la Ubungo Prof. Kitila Mkumbo sambamba na Madiwani wote wa Kata kupitia Chama cha Mapinduzi CCM wanaibuka na ushindi Mkubwa.








🚨Subscribe YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post