SAMIA KUCHUKUA FOMU YA URAIS AGOSTI 9, KIPENGA CHA KAMPENI CHA PULIZWA

 


Na Jasmine Shamwepu Dodoma.


MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi CCM,Taifa ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan Agosti 9 Mwaka 2025 atachukua Fomu ya Mgombea nafasi ya Urais kwa Tiketi ya CCM katika Ofisi za Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)


Zoezi la uchukuaji wa fomu linaashiria wazi kupulizwa rasmi kwa kipenga cha Kampeni kwa Vyama vyote vya Siasa katika kushiriki uchuguzi Mkuu ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba 29 Mwaka huu.


Katibu wa Itikadi,uenezi na Mafunzo wa Chama hicho,CPA Amos Makalla ameyasema hayo leo Agosti8Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na mchakato wa uchukuaji fomu za Wagombea.


Pamoja na mambo mengine,CPA Makalla amebainisha kuwa, kwasababu Mgombea wa nafasi ya Urais anatokana na Chama cha Mapinduzi, baada ya hapo wanatarajia kumpokea katika Ofisi za CCM Makao Makuu Dodoma na baada ya hapo atapata fursa ya kusalimiana na wananchi.


Ikumbukwe kuwa Rais Dokta Samia anachukua fomu ya Mgombea Urais kwa kipindi kingine cha Miaka mitano ambayo ni awamu ya pili ili kukamilisha uongozi wake.




🚨Subscribe YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA

Previous Post Next Post