Wellu Mtaki, Dodoma .
Nyasi asili inayokua kwenye maeneo ya jangwa au nusu jangwa na kupandwa kwenye maeneo yenye ukame Ant grass inasaidia kukuza Mifugo aina ya Ng'ombe.
Hayo yamebainishwa na Afisa Uvuvi wa halmashauri ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida Pascal Maiko Peter wakati akizungumza na vyombo vya habari Jijini Dodoma Katika maonesho ya nanenane huku akiwataka wananchi kutembelea Banda la halmashauri hiyo kujionea Ng'ombe mwenye kilo zaidi ya 1000 anayeleta maajabu Katika maonesho hayo.
Amesema licha ya Mifugo ya Ng'ombe pia wapo Mifugo mingine ikiwemo Ufugaji wa samaki, kuku, Bata pamoja na Sungura.
"Ant grass" kwa malisho ya Ng'ombe kwa kawaida humaanisha nyasi aina ya Anthephora pubescens - nyasi ya asili inayokua sana kwenye maeneo ya jangwa au nusu jangwa, hasa kusini mwa Afrika, lakini pia hupandwa kwenye maeneo yenye ukame kama malisho" amesema.
Aidha ameeleza kuwa mkoa wa Singida hakuna ziwa Wala mito ila wanatumia mabwawa kwa ajili ya Ufugaji wa samaki na kusaidia kupata maendeleo endelevu kwa kujiongezea kipato kwa mtu mmoja mmoja na kuondoka umasikini .
Mbali na hayo amesema kuwa huduma ya chanjo inapatikana bure kwa mteja ambaye atachukua Mfugo aina ya kuku hivyo amewaasa wafugaji kutembela Banda hilo Ili kupata Elimu zaidi.
🚨Subscribe YOUTUBE Channel Yetu ya WASHINDI MEDIA.