MABALOZI WA TANZANIA NA BOTSWANA WAKUTANA MAPUTO, WAWEKA MIKAKATI YA KUONGEZA BIASHARA NA UWEKEZAJI


 24 Julai 2025 – MAPUTO: Mhe. CP. Hamad Khamis Hamad, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini  Msumbiji amekutana na Mhe. Chandapiwa Nteta, Balozi wa Jamhuri ya Botswana nchini Msumbiji kwa ajili ya kujitambulisha.


Viongozi hao pia walizungumza masuala mbalimbali ya uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo na vilevile masuala ya ushirikiano ya Kikanda (Regional Cooperation), hususan ushirikiano kwenye Jumuiya ya SADC. Aidha, Viongozi hao walikubaliana kufanya kazi kwa ukaribu ili kufanikisha malengo ya nchi zao kwa muda woye wakiwa nchini Msumbiji.


Viongozi hao kwa pamoja walieleza kuridhika kwao na uhusiano kati ya nchi zao mbili, hata hivyo walisisitiza juu ya haja ya kuimarishwa uhusiano kwenye sekta ya uchumi huku msukumo mkubwa ukiwekwa kwenye kuongeza kiwango cha biashara na uwekezaji.



Previous Post Next Post