CHATANDA AMLILIA MAREHEMU ANNA LUVANDA "MAMA MAKETE"

 



Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT), Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) Leo Tarehe 22 Julai, 2025 amefika nyumbani kwa Marehemu  Anna Hangaya Luvanda maarufu, (Mama Makete) aliyekuwa Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kinondoni, Maeneo ya Nyakasangwe,Wazo Hill Wilayani Kinondoni Jijini DSM, Na Kuungana na Familia, Ndugu, Jamaa, na Wanachama wa UWT/CCM kwa kutoa pole kufuatia Kifo hicho.


Mama Makete alifariki Dunia Jana Tarehe 21 Julai, 2025, Mchana akiwa katika Hospitali ya Hindu Mandal alikokuwa akipatiwa matibabu kutokana na Matatizo ya kiafya, na anatarajiwa kuzikwa siku ya Alhamisi Tarehe 24 Julai, 2025 Nyumbani kwake Wazo Hill Jijini DSM.




#pumzikakwaamaniAnnaLuvanda

Previous Post Next Post