Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT), Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) ameshiriki mazishi ya Ndg. Lucia Sulle aliyekuwa Katibu wa UWT Mkoa wa Mbeya iliyofanyika Wilayani Babati leo tarehe 03 Aprili, 2025.
Aidha,Mwenyekiti wa UWT Taifa aliambatana na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Taifa, ambapo ibaada hiyo imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi Taifa wakiwemo Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi Taifa, Wajumbe wa HalmashauriKuu ya CCM Taifa, Uongozi wa CCM Mkoa wa Manyara pamoja na Viongozi wa Serikiali kutoka Maeneo mbalimbali ya Tanzania wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga.
Tags
HABARI