UZINDUZI WA KWAYA YA RIHOBOTHI MCH. KIBONA AONGOZA IBADA YA KUWEKA WAKFU

 


Na Carlos Claudio, Dodoma


Kanisa la Moravian Tanzania limewataka Waumini  wake kutokuwa na hofu wanapokumbana na changamoto badala yake wawe na amani moyoni kwani hata maandiko yanaeleza namna Yesu aliwaonekania wanafunzi  wake na kuwaambia amani iwe kwao.


Hayo yameelezwana leo Aprili 27,2025 jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Kanisa hilo Jimbo la Kaskkazini Mchungaji. JEREMIA KIBONA katika Ibada ya uzinduzi na kuwekwa wakfu kwa jina la REHOBOTHI CHOIR ya Moravian Mkonze jijini Dodoma.


MCH. JEREMIA amewataka vijana kuruhusu Yesu aishi ndani yao kwani inapelekea kuwepo kwa amani katika taifa na kupunguza matukio ya kuwaumiza wengine hasa wazazi. 



Nao baadhi ya washirika wa Kanisa hilo wamemshukuru Mungu kwa hatua kubwa ikiwemo uzinduzi na kuwekwa wakfu kwa kwaya hiyo huku baadhi ya wanakwaya wameeleza changamoto mbalimbali walizokumbana nazo ambazo hazikuwakatisha tamaa.


Jina la REOBOTHI linapatikana katika kitabu cha mwanzo sura ya 26 msitari wa 22 kwa muktadha huo, Isaka alikuwa anakutana na upinzani kila alipochimba visima, Lakini alipofika mahali ambapo hakukuwa na ugomvi, aliita kisima hicho REHOBOTHI maana yake Mungu ametutengenezea nafasi.











🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post