KUKOSOA PEKEE HAKUIFANYI CHADEMA KUWA MBADALA WA ССМ- МСН. MSIGWA

 


Kada wa Chama Cha Mapinduzi Mchungaji Peter Saimon Msigwa ameeleza kuwa Kukosoa huenda ikawa ni miongoni mwa kazi za Vyama vya upinzani kote duniani, akitahadharisha wanachama wa Chadems kuwa kazi hiyo pekee kama inavyofanywa na viongozi wao haiwezi kukipa sifa yoyote ya kuwa chama mbadala cha kuunda serikali kwa kuitoa CCM madarakani.


Wakati wa ziara ya siku tano ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi Mkoani Mara, @pmsigwa_ameeleza kuwa ni ndoto kwa vyama vya upinzani kuweza kutegemea kushika dola na kuiondoa CCM madarakani kwa kutegemea udhaifu wa Chama hicho badala ya uwezo wake binafsi, akisisitiza kuwa nchi ipo salama chini ya CCM ya Dkt. Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu Dkt. Nchimbi.


"Kama manzania mzalendo, tuna nchi ya kuijenga ambayo ni Tanzania na nimejiunga na jeshi la Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha nchi inazidi kwenda mbele na niwahakikishie kwamba

nchi itapaa chini ya Dkt. Samia na zawadi pekee ninayoomba muwape ni kumpatia kura za kutosha Dkt. Samia na Balozi Nchimbi kwenye uchaguzi wa mwezi Oktoba." Amesema Mch. Msigwa.


Kulingana na Mch. Msigwa akiwanukuu waandishi mbalimbali wa sayansi ya siasa ameeleza kuwa katika siasa zipo nadharia mbili pekee zinazoongoza watu katika kuchagua chama au mgombea fulani katika mazingira ya upinzani, moja ikiwa ni kushindanisha sera na nyingine ya pili ikiwa ni imani kwa chama au mgombea, suala ambalo amekiri wazi kuwa hakuna nadharia miongoni mwa hizo mbili yenye kuonekana kufanya kazi kwa Chadema.


Msigwa pia akizungumzia maendeleo mbalimbali yaliyoshuhudiwa kwa miaka minne ya ongozi wa Rais Samia, amebainisha kuwa mafanikio hayo yamewakosesha zaidi upinzani ajenda za kuzungumza, akiwajibu baadhi ya watu kwa kusema kuwa anaambatana na viongozi mbalimbali wa CCM baada ya Nuru kumuwakia na hivyo dhamira yake ni kuwakatisha tamaa wanachama wa Chadema kwa kuwaeleza ukweli kwamba wanapoteza muda kukiunga mkono chama ambacho kimepoteza mwelekeo na kisichokuwa na dira.

Previous Post Next Post