Dar Es Salaam.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimesema mpaka kufikia hivi sasa hakina taarifa za alipo mjumbe wa Baraza Kuu la chama hicho Hilda Newton baada ya kukamatwa siku ya jana akiwa eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar Es Salaam.
Akizungumza na vyombo vya habari leo April 25, 2025 Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho bara Amani Golugwa amesema "Tuna mwanachama wetu ambaye ni mjumbe wa baraza kuu Bi Hilda Newton kama ofisi zetu za chama hatuna taarifa zozote zilizo rasmi zinazoonyesha kwamba hilda Newton yuko wapi."
Golugwa amedai kuwa Hilda alikamatwa eneo la Kisutu na walitegemea kuwa taarifa ya jeshi la Polisi iliyotoka jana pengine ingekuwa na jina la mjumbe huyo "Jana kwenye taarifa ambayo afande Muliro alitaja majina ya viongozi na wanachama ambao wapo kwenye mikono ya jeshi la Polisi.
Na pia alitoa taarifa kuhusiana na mtu mmoja ameokotwa kwenye ufukwe wa Coco Beach taarifa ya Hilda Newton kuwa kwenye mikono ya polisi haikutolewa."
🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.