OFISI YA MKAGUZI NA MDHIBITI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA RUKWA


Waandishi wa habari wametakiwa kuripoti na kutekeleza majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuijuza jamii kuhusu utendaji kazi wa Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali bila kuvunja maadili na miiko katika uandishi na uwasilishaji ili kuondoa sintofaham kwa wananchi. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari hii leo July 22,2024 wakati akitoa mafunzo kwa wanachama wa Club ya waandishi wa habari Mkoani Rukwa kwenye Warsha iliyofanyika katika ukumbi wa Libori uliopo manispaa ya Sumbawanga Focus Mauki ambaye ni Mkuu wa kitengo Cha mawasiliano serikalini amesema ili kuwezesha wanahabari kufanya kazi kwa weredi na ufanisi ofisi ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali itahakikisha inashirikiana na wanahabari na wadau wengine ili kurahisisha upatikanaji wa habari.

Mauki amesema lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuhakikisha kuwa waandishi wa habari wanapata elimu na uelewa wa kutosha kuhusu utendaji kazi wa ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali ( CAG).

Aidha Mauki amesema ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) imejidhatiti katika kuimarisha masuala ya usimamizi utawala na maadili pamoja na kuwa na mawasiliano kati ya ofisi hiyo na wadau wengine.

Nae mwezeshaji kutoka ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali kitengo Cha huduma za kiufundi Happy Mlingi amesema lengo la ofisi ya CAG ni kuhakikisha Wana wajengea uwezo wadau mbalimbali ili wawe na uelewa wa kutosha na kufanya kazi kwa misingi ya uwajibikaji huku akisema ofisi inaimarisha masuala ya rasilimali watu na taaluma kwa watumishi.

Nswima Ernest ni Mwenyekiti wa Club ya waandishi wa habari Mkoa wa Rukwa  ameishukuru ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali kwa kuwapa mafunzo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi huku akitilia mkazo suala la ushirikiano.  

Awali akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Libori center Manispaa ya Sumbawanga Mkaguzi Mkuu wa nje (CEA) Mkoa wa Rukwa Thomas Lumbillah amesema atahakikisha kunakuwepo na ushirikiano kati ya ofisi ya CAG na wadau mbalimbali ili kurahisisha utendaji kazi wa ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) hali ambayo itasaidia kupunguza mianyaya upotevu wa fedha za umma.



Previous Post Next Post