AMUUA MDOGO WAKE KISA KUUZA MBUZI AMTIBU MAMA YAKE MZAZI


Na.Fedrick Mbaruku-Rukwa

MWANAFUNZI mmoja wa darasa la saba aliefahamika kwa jina la Pius Chakupewa (10) ameuawa na kaka yake aliyefahamika kwa jina la Samwel Chakupewa anaekadiliwa kuwa na umri zaidi ya miaka (35) baada ya kutokea kwa mvutano wa KIfamilia.

Tukio hilo limetokea April 27,2024 majira ya saa 11 jioni katika kijiji cha Masolo kata ya kipili wilaya ya Nkansi Mkoani Rukwa.

Kwa mjibu wa taarifa ya Mwenyekiti wa kijiji cha Masolo wilayani humo Ndg.Joackm Albeto Mbalamwezi amesema marehemu alikuwa amefuga mifugo yake (Mbuzi) wapatao 9 baada ya mama wa marehemu kuugua alipelekwa katika kituo cha afya Kilando kwa ajili ya matibu.

“Yule mwanafunzi alikuwa amefunga mbuzi 9 baada ya mama yao kuugua marehemu aliuza mbuzi mmoja alivyouza badae akamwambia mama yake auze mbuzi wa pili waendelee na huduma mama yake akasema hamna shida basi akawa amechukua akauza.

“Kaka wa marehemu Samwel akamuuliza kwanini unauza mbuzi? marehemu akasema mimi nauza kwa sababu ya mama aweze kutibiwa Samweli akasema kwa hiyo wewe umenizidi akili kisha kumbeba kijijini maana walikuwa wanaishi shambani walivyofika akamuingiza ndani na kuanza kumshambulia na mti,”amesema Mwekiti Joackm Albeto Mbalamwezi.

Mwenyekiti huyo amesema Samwel Chakupewa ambae ni mtuhumiwa amemshambulia marehemu katika sehemu mbalimbali za mwili wake hasa kichwani kwa kutumia mti hali iliyo pelekea kifo hicho huku ikielezwa kuwa mtuhumiwa huyo amewahi kutishia kumua mke wa shemeji yake.

Amesema baada ya kutokea kwa tukio hilo wananchi wema wameshirikiana kumtafuta mtuhumiwa huyo baada ya kufanikiwa kumpata wamemfikisha katika kituo cha polisi ili kuendelea na shughuli za kiuchunguzi huku akiitaka jamii wilayani humo na mkoa kwa ujumla kufanya mabadiliko kwa kushauliana pindi inapotokea migogoro katika jamii.

Kwa upande wa Dada wa marehemu Cesilia Osca Chakupewa amesema chanzo cha tukio hilo ni marehemu kuuza mbuzi wake kwa lengo la kumtibu mama mzazi ndipo kaka yake aliingilia kati kuzuia marehemu asiuze mifugo hiyo.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoani humo linaendelea shughuli za kiuchunguzi kufuatia tukio hilo.

(Tafadhari endelea kufuatilia Blog yetu tutakuletea undani wa taarifa hii hapo badae Mhariri Fedrick Mbaruku).

Previous Post Next Post