📌Asisitiza Wazazi kuwapeleka Watoto Shuleni.
📌Aonya wazazi wanao waficha wanafunzi wenye ulemavu.
📌Atoa maagizo kwa wakuu wa Wilaya.
Na.Fedrick Mbaruku-Rukwa
"Wazazi watakao wakosesha watoto haki yao ya elimu ya msingi ikiwa ni pamoja na kuwaoza wale wanaoanza kidato cha kwanza wachukuliwe hatua kali za kishelia ili kukomesha tabia ya kuwaoza watoto badala ya kuwasomesha.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe.Makongoro Nyerere ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka watoto kujiunga na elimu ya awali na kidato cha kwanza ili kupata haki yao ya Elimu.
Mhe.Makongoro ametoa wito huo leo January 8,2024 wakati akitoa tathimini ya maendeleo ya Mkoa katika sekta ya elimu mbele ya Waandishi wa Habari katika ukumbi mdogo wa mikutano Mkoani humo.
Akitoa tathimini hiyo amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia kupitia mpango wa BOOST Imetoa kiasi cha fedha shillingi Bilioni 6,64 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya tisa na ujenzi wa madara ya awali nyumba za walimu na vyoo katika shule za msingi 20.
Amesema serikali imetambua umhimu wa kufanya maboresho ya miundombinu ya shule na kusema zaidi ya shilingi Bilioni 5.9 na milioni 900 zilitolewa na serikali zitumike katika ujenzi wa shule mpya za sekondari ambapo kati ya shule hizo 5 ni za sekondari za kata na moja ni Mkoa.
"Mpaka sasa shule hizo nne za sekondari zimekamilika na zimekwisha sajiliwa,kukamilika kwa shule hizo kutapunguza adha kwa wanafunzi kutembea muda mrefu kufika shuleni.
"Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu tunashuhudia madarasa yakiwa teyari yameshajengwa yanasubili wanafunzi huko nyuma wanafunzi walikuwa teyari madarasa bado hayajajengwa.
Mhe.Makongoro amesema Mkoa ulilenga kuandikisha wanafunzi wa elimu ya awali 57,006 ikiwa wakiume ni 27,885 na wakike ni 29,121 ambapo hadi kufikia mwezi January 4,2024 wanafunzi 24,033 wa darasa la awali 42.1% .
Pia amesema kwa upande wa darasa la kwanza Mkoa ulilenga kuandikisha wanafunzi 51,347 wakiume wakiwa ni 25,254 na wakike ni 26,093 ambapo hadi Januaari 4,2024 jumla ya wanafunzi 30,922 sawa na 60.2% waliandikishwa kujiunga na darasa la kwanza.
Aidha amebainisha idadi ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu ambapo amesema takribani wanafunzi wa elimu ya awali ni 167 kati ya hao wakiume ni 169 na wakike ni 98 wameandikishwa hadi kufikia Januari 4,2024 na upande wa darasa la kwanza wanafunzi wenye mahitaji maalumu ni 91 wakiume wakiwa ni 43 na wakike 48 walikuwa wameandikishwa hadi kufikia January 4,2024,"Mhe.Makongoro.
Pia amesema kwa upande wa sekondari jumla ya wanafunzi 31,182 walifanya mtihani na kuhitimu darasa la saba 2023 ambapo kati yao wavulana ni 13,946 na wasichana ni 17,236 sawa na 97.2% wa wanafunzi walioandikishwa.
Amesema baada ya matokeo watahiniwa 24,415 wavulana wakiwa ni 11,270 na wasichana 13,145 sawa na 78.3 walifanya vizuri na kuchaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari kwa mwaka 2024 katika shule mbalimbali za Mkoni humo ikiwa ni pamoja na shule za kutwa,bweni,ufundi na vipaji maalumu zilizopo nje ya Mkoa wa Rukwa.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo ametembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule mbili Msingi na Sekondari Mkoani humo huku akipongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita katika kuendelea kuimalisha ujenzi wamiundombinu mbalimbali hapa nchini.
Mhe.Makongoro ameonya suala la wazazi kuwafungia wanafunzi wenye ulemavu badala yake kuwapa kipaumbele cha kuandikishwa elimu ya awali na msingi huku akiwataka wakuu wa Halmashauri zote Mkoani humo kuhakikisha wanakusanya taarifa za uandikishaji wa wanafunzi.
Sanjali na hayo Mkuu huyo ameagiza kuchukuliwa kwa hatua za kisheria wazazi watakao shindwa kuwapeleka watoto shuleni kwa sababu za kuwaozesha na hivyo kuwanyima haki zao za msingi.
"Watoto wa kike wanahaki ya kutimiza ndoto zao kama watoto wa kiume,wanafunzi wapokelewe bila masharti yoyote hakuna ada katika shule za sekondari,"amesema Mhe.Makongoro.
MWISHO.