RAIS SAMIA AONDOWE WAZO KUHUSU FOMU YA URAIS:MTETEZI WA MAMA RUKWA

Na,Fedrick Mbaruku-Rukwa

KATIKA kuelekea mwaka mpya wa 2023,Viongozi wa Taasisi ya Mtetezi wa Mama Mkoa wa Rukwa wamefanya mkutano na Waandishi wa Habari uliolenga kuitangaza rasmi Taasisi na kujadili shughuli mbalimbali za kimaendeleo zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Awali akizungumza Mwenyekiti wa taasisi hiyo Alex Philimoni amesema Taasisi hiyo imeadhimia kumchangia fedha za fomu ya Urais kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2025.

Mkutano huo umefanyika leo Desemba 30,2023 katika ofisi zilizopo mkabala na Benk ya NMB Manispaa ya Sumbawanga Mkoani humo ambapo wameyabainisha manufaa yaliyopatikana ndani ya kipindi cha uongozi tangu aingie madarakani.

Amesema katika kipindi cha miaka mitatu yapo mengi yaliyofanywa na Dkt.Samia ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa miundombinu mbalimbali katika halmadhauri zote nchini ikiwemo miradi ya ujenzi wa shule,vituo vya afya na vifaa tiba,maji,umeme,maboresho ya viwanja vya ndege kikiwemo kiwanja cha ndege kilichopo Manispaa ya Sumbawanga Mkoani humo pamoja na kushusha gharama za pembejeo za kilimo hali inayochangia kukua kwa pato la Taifa.

“Yapo mengi tukianza kuyataja hapa tutafika kesho kwahiyo tuna kila wajibu wa kuyasema mengi yanayofanywa na Mama yetu Dkt.Samia mfano mzuri ni ujenzi wa kiwanja cha ndege katika Mkoa wetu huu,boti za kisasa,barabara,Geneleta ya umeme wa zaruru katika kituo cha afya mazwi na mengine mengi,”amesema Philimoni.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Deborah Endruw amesema kutokana na kuongezeka kwa miundombinu  mbalimbali kwa kuongeza vituo vya afya na vifaa tiba imesaidia kupungua kwa vivyo vya mama na mototo vilivyokuwa vikiwakabili watu wengi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Previous Post Next Post