Na Fedrick Mbaruku
Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam limewatahadharisha wananchi waliopanga kufanya maandamano yaliyoandaliwa na mtu mmoja ambaye hajatajwa jina lake kwenda Ikulu ya Magogoni Jijini Dar es salaam siku ya juma tatu Juni 19,2023.
Taarifa hiyo imetolewa leo Juni 17, mwaka huu na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Jumanne Muriro amesema taarifa hiyo aliyodai kuwa alifikisha mahakamani teyari imejibiwa kwa kuyapiga marufuku maandamano hayo na kumtaka afuate kanuni na taratibu za kisheria ili haki iweze kutendeka na wananchi waendelee na shughuli zao za kiuchumi.
Aidha Jeshi la Polisi Mkoani humo limeowatahadharisha na kuonya vikali kwa watakao shiriki na kusema jeshi halitasita kuchukua hatua kwa atake bainika kujihusisha na hicho kinacho tajwa kuwa ni maandamano.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dae es Salaam limefanikisha kuwakamata watuhumiwa 10 kwa tuhuma za kuhujumu miundombinu ya vifaa mbalimbali vya minara ya mawasiliano ya simu.
Taarifa hiyo imetolewa leo Juni 17,2023 na Kamanda wa Jeshi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Jumanne Murilo ambapo amesema Kukamatwa kwa watuhumiwa hao ni mala baada ya Jeshi hilo kufanya Oparesheni maalumu iliyoanza Juni 5,mwaka huu huku jeshi likiendelea na Oparesheni hiyo katika mikoa ya jirani na Jiji la Dar es salaam.
Jeshi hilo limeyaainisha baadhi ya majina ya watuhumiwa hao akiwepo Husein Ally Kijinga (32) mkazi wa Mbande Kisewa,Simon Mangu (33) mkazi wa Ubungo,na mwenzake mmoja baada ya kukutwa na vifaa hivyo vinavyoibwa na kuhifadhiwa katika eneo la Mbezi Luis wakiwepo na wenzake 7 ambao wamekuwa wakitekeleza vitendo vya wizi wa betri muhimu na vifaa mbalimbali vya minara ya mawasiliano ya simu katika maeneo mbalimbali Jijini humo.
Takribani betri 68 zenye thamani ya shilingi 153.200,000 na vifaa vingine vya minara ya mawasiliano ya simu vilivyo ibwa magari 2 yanayotumiwa na watuhumiwa hao yamekamatwa likiwemo gari aina ya Toyota Ililus lenye namba za usajiri T.850 BDR,Toyota Carina T112 BRN na pikipiki mc.901 DJQ pamoja na vifaa mbalimbali vya kuvunjia.